TOLEA UHAI


Utengenezaji Shirikishi wa Ruzuku 

 Jamii zetu kupitia ruzuku mahirimu na mikakati zimetambua masuala ya kufadhili na kutoa fedha milioni 12 Dola za Marekani katika ruzuku 900. Mwelekeo huu unabadilisha maamuzi yanayofanywa yawe ya kuendeshwa na jamii wala si mfadhili. Ni mwelekeo  mwangalifu kifyake kwa kuwa jamii zinajua ni nani anafanya kazi gani. Hatimaye, inaturuhusu kubahatisha sehemu ambapo kwa muda mrefu wafadhili wamekwepa.
Utengenezaji shirikishi wa ruzuku unaturuhusu kuzingatia makundi mseto na kufikia kila makundi ambayo yangesahaulika na wafadhili wakuu kama vile transijenda, huntha, wakimbizi au jamii wahamiaji za jinsi na jinsia zilizotengwa.
 

Utetezi wa Kihisani

Kupitia utetezi wa kihisani, UHAI limeshiriki kiuamilifu katika kubadilisha jinsi ufadhili wa mavuguvugu unavyofanywa katika viwango vya kitaifa na kikanda. UHAI EASHRI linasaidia kanda nyingine katika Afrika kuanzisha hazina sawia ijulikanayo Initiative Sankofa d’Afrique de l’Ouest (ISDAO) na pamoja na washirika wetu katika Love Alliance.
UHAI linatengeneza 1 kwa kila ruzuku 6 ya jamii ya jinsi na jinsia zilizotengwa duniani, na lipo katika nafasi ya 9 ulimwenguni kama mfadhili mkubwa wa haki za wafanyakazi wa ngono.

Toa na Usaidie 

Mchango wako unahakikisha jamii za jinsi na jinsia zilizotengwa na wafanyakazi ngono kutoka pande zote za Afrika Mashariki zinasaidiwa ili kudumisha vita katika dunia ambapo watu wote waishi kwa usawa na hadhi.
Mchango wako unahakikisha jamii za jinsi na jinsia zilizotengwa na wafanyakazi wa ngono katika Afrika Mashariki zinapokea usaidizi zinazohitaji ili kukuza unyumbukaji na kuleta mabadiliko ya jamii. Jiunge na vuguvugu kwa ajili ya vita vya kuleta usawa katika AFRIKA Mashariki kwa kutoa michango kila mwezi.