KUHUSU UHAI

 

MASUALA YETU 

UHAI - EASHRI ni wanaharakati wahisani katika kanda ambapo utambulisho wetu kama watu wa LGBTIQ+ na kama wafanyakazi wa ngono umeharamishwa kupitia sheria zenye adhabu kali, ambapo serikali zinafunga kiuamilifu nafasi za vuguvugu zinazoratibu kumaliza ubaguzi katika ufikiaji wa huduma na utunzaji afya, ambapo maoni ya jamii na umma hudumisha utengaji kutoka kwa familia, kutoka kwa jumuiya za imani na kunyimwa haki za msingi kama vile ufikiaji wa maisha yenye hadhi, ufikiaji wa kusikizwa bila mapendeleo na haki na vyombo vya madola.

 

NJIA ZETU

Njia zetu za kufanya kazi zimejumuishwa pamoja katika maadili yetu inayowakilishwa na neno la Kiswahili linalounda jina letu. Hizi juhudi zetu zisizodhurika  zinadhihirisha utambulisho wetu na jinsi tunavyoshirikiana na jamii zetu na jumuiya wanamoishi.


UHAI linatoa ufadhili nyumbufu na usaidizi wa uwezo kiitikio kwa jamii za jinsi na jinsia zilizotengwa na wafanyakazi wa ngono, na linasaidia katika utafiti, ushirikianaji na kuratibu makongamano ya Afrika Nzima. Kwa kuwashirikisha wanaharakati wa ndani ili kuamua utengenezaji wa ruzuku zetu, mtazamo wetu wa mabadiliko ya kijamii unahakikisha kuwa wale wanaoishi katika mapambano wana wakala wa kufadhili shughuli.

 

WATU WETU

UHAI linaongozwa kiuwanaharakati, huku ni kumaanisha linatawaliwa kiuwanaharakati, wafanyakazi wake ni wanaharakati. Neno Asili halimaanishi tu kiukanda au ndani kwetu sisi, pia linamaanisha wanaharakati ambao maisha ya uhalisia ni ya kupambania jamii zetu katika kanda hii, inaongoza juhudi na kazi zetu za UHAI.

 

HADITHI ZETU

 

VIDEO ZA UHAI

 UHAI - EASHRI linazungumzia ushirikianaji na video kuhusu mada kadhaa

 

SAUTI ZA UHAI

UHAI - EASHRI limeweka sauti za jamii kwa podikasti kuhusu mada kadhaa

 

VIJARIDA VYA UHAI

UHAI - EASHRI limehifadhi nyaraka zetu zote za vijarida

 

BLOGU ZA UHAI

Cleo Kambugu in November 2022 finally got an ID that recognizes her gender. Cleo is a transgender activist in Uganda and she says she hopes that this civilian win for her will translate into more civic movement victories.