UFUNDISHAJI NA UANDAMIZI

UFUNDISHAJI NA UANDAMIZI

UHAI inawaimarisha waruzukiwa katika usimamizi wa kifedha na wa kishirika kupitia kwa mchakato wa udhamini wa kifedha kwa wabia waruzukiwa wanaoibuka  kupitia kwa mashirika mahirimu  yaliyokomaa. Mpangilio huu unayaruhusu mashirika yanayodhaminiwa kifeha kupata stadi za kiutendaji na tajiriba katika usimamizi wa kifedha wa kimsingi wanapotekeleza ruzuku zao kutokana na  kukumbana na michakato ya kifedha ya mdhamini wao.


UHAI inafanikisha ufundishaji na ulezi ambapo mashirika wadhamini wanajenga maarifa na stadi mpya miongoni mwa mashirika waruzukiwa kwa kukuza ufanisi katika taratibu za kifedha na mifumo kwa usimamizi fanisi wa ruzuku.


UHAI pia inatoa uandamizi kwa waruzukiwa wetu wakati wa uwekaji mkataba wa ruzuku, matembezi kabla ya utekelezaji na usimamizi wa ruzuku. Wafanyakazi wa UHAI pia wanawafundisha wabia waruzukiwa walio na upungufu kuhusu mapengo yaliyobainishwa wakati wa ukadiriaji shirikishi wa uwezo unaonuiwa katika kujenga stadi mahsusi za kiufundi katika usimamizi wa kifedha, upangaji, kuunda mitandao, kuweka bajeti na kuchangisha rasilmali.