Knowledge and Learning

Kupitia kufadhili na  kuendesha utafiti  na vile vile kongamano la  Changing Faces Changing Spaces, tunaumba vifaa na nafasi za kufanikisha wanaharakati kutoa sauti kwa mazingira ya wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakzi ya ngono  kwa kuwasilisha tajiriba za upangaji na utetezi, kufuatilia mielekeo na kujenga miungano na wakati huo huo kutupatia mafunzo kuhusu mabadiliko na mahitaji yaliyopo.

Changing Faces,Changing Spaces

Changing Faces,Changing Spaces

Mwaka 2007, kongamano la uanaharakati lenye maudhui “Changing Faces Changing Spaces” (CFCS) liliendeshwa na wachache wa ujinsia na jinsi ana wafanyakazi ya ngono na marafiki na wafadhili wao. Mkutano huu ulitambua tofauti zisizoweza kutatuliwa baina ya ulimwengu wa kifedha unaoathiriwa na umagharibi na ulimwengu wa kikazi katika kanda hii. Hitimisho la mkutano huo ulikuwa kwamba palihitajika utaratibu wa ufadhili unaoongozwa na wanaharakati wa kijamii katika mashirika ili kuziba pengo baina ya ufadhili na kazi.

Miaka miwili baadaye UHAI ilizaliwa pamoja na mtazamo shirikishi wa utoaji ruzuku ili kufadhili ujenzi wa mashirika katika kanda hii. Tangu wakati huo, UHAI imeendesha CFCS kila baada ya miaka miwili ambao umekua katika utambulisho wake wa Uafrika. Mwaka 2019,UHAI iliendesha CFCS kwa mara ya 7 na kuendeleza utamaduni wa CFCS kama jukwaa ambalo wanaharahaki wa haki za binadamu na mashirika, wataalamu wa afya na sheria, marafiki na wafadhili wabia kutoka Afrika nzima  na nje wanaendesha na  na kuunga  mkono uanaharakati wa wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakazi ya ngono wa Kiafrika kwa kujadili, kuweka mikakati na kubadilishana tajiriba ambazo zinaathiri mashirika yetu.

Katika kufuatilia utamaduni wetu wa ushirikishi , kongamano hili lilizuliwa na kupangwa na jopokazi la wanaharakati kutoka kwa mashirika ya walio wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakazi ya ngono katika Afrika.

Kwa habari kuhusu CFCS inayofuatia na kuongezwa kwenye orodha ya anwani ya CFCS tafadhali tuandikie barua pepe katika cfcs@uhai-eashri.org au  roselyn@uhai-eashri.org.

SHARE YOUR EXPERIENCES