KUWA SAUTI

BE
THE VOICE

for us, by us

for us, by us

Ruzuku za UHAI zinaamuliwa na wanaharakati wa kijamii ambao wanaishi katika jitihada husika z kila siku.

1. KWANZA

UHAI ni ufadhili wa kwanza kwa mashirika mengi ya uanaharakati katika Afrika ya Mashariki. Tunachukua hatari muhimu ili kufadhili mawazo yanayahidi na mashirika ambayo hayafahamiki kwa wafadhili wengine na kuchangia katika kujenga mashirika yetu.

2. UAMINIFU

UHAI inadumisha ufadhili kwa wabia wetu katika miaka , pamoja na usaidizi wa uwezeshaji ili kukuza uadilifu wa kimiundo. Kupitia kwa ufadhili wa kimsingi na wa miaka kadha, tunawezesha mashirika kudumisha mipango na kupata mabadiliko ya muda mrefu.

3.NYUMBUFU

UHAI haiamui kimbele maeneo ya ufadhili mbali inafadhili mahitaji ya kisasa na ya kidharura kama yanavyotambulishwa na wanahakarakati. Na, tunafahamu kwamba mashirika yote hayajasajiliwa rasmi –hasa katika miaka ya mwanzo –na kwa hiyo tunazingatia maombi bila kujali hadhi ya usajili. Kati hali kama hii, tunatoa ufadhili kupitia wadhamini wa kifedha katika mashirika yetu.

grants

grants

Ruzuku za uhai zinaamuliwa na wanaharakati wa kijamii kutoka kwa mashirika ya wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakazi ya ngono . Katika kuitikia mahitaji ya mashirika , UHAI inatuza Ruzuku za Mahirimu kupitia mzunguko wa wito wa maombi ya mara moja kwa mwaka na Ruzuku za Nafasi , Kimkakati na Uwezeshaji kwa misingi yaa kuendelea

Wakati mashirika yetu yanazidi kukua, mahitaji yao yanazidi kuongezeka . Kwa kuongezea, hivi leo tofauti na hapo awali, mazingira yanazidi kuwa ya uadui na vurugu. Hivyo UHAI inapigania ufadhili wa kuendelea na wa kuongezeka ambao tunaweza kutoa kwa mashirika yetu .

NI AINA ZIPI ZA RUZUKU AMBAZO NINAWEZA KUOMBA?

UHAI inatuza Ruzuku Mahirimu kupitia kwa mwito wa maombi wa mara moja kwa mwaka na Ruzuku za Fursa, Kimkakati na Uwezeshaji kwa misingi wa kuendelea

NI NINI MNACHOZINGATIA?

UHAI ni ufadhili nyumbufu na unaoitikia. Hatuamui kimbele maeneo ya kufadhili.

NANI ANAAMUA?

Ruzuku Mahirimu yanaamuliwa na Kamatiya Ruzuku Mahiriku (PGC). Ruzuku za Kimkakati, Fursa na Uwezeshaji zinaidhinishwa na Wakurugenzi Wakuu Wenza kwa mapendekezo ya Kamati ya Ruzuku ya Ukatibu wa UHAI (SGC).

capacity support

capacity support

Mazingira ambao wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakazi ya ngono wa Afrika ya Masharika wanafanyia kazi ni banifu na inaweka vikwazo vikuu kwa upangaji fanisi. Mwanzo, mahitaji ya mashirika kutenda kazi yakiwa mafichoni inamaanisha kwamba mara nyingi hayawezi kupata rasilmali muhimu za kuendelea kama mashirika ya kawaida.
Kuimarisha uwezo huu umekuwa wa kimsingi kwa UHAI. Tunaandama ruzuku kwa uwezeshaji ili kujenga uwezo wa shirika na wa uongozi na ufanisi wao. Tunaamini kwamba uwezeshaji ni muhimu sawa na ufadhili katika kukuza uanaharakati ambao unawasilisha kwa uwazi, ulio na maarifa, ulio endelevu na unaowajibika. Mtazamo wa uwezeshaji wa UHAI unajumuisha mshirika kwanza kutafsili ajenda yake ya kujifunza na kutokana nao tunaweza kufanikisha ujifunzaji wa mahirimu ndani ya mashirika yetu ama kutoa ulezi wa moja kwa moja.

UFUNDISHAJI
UANDAMIZI

Ufundishaji na uandamizi unatolewa kwa wabia waruzukiwa katika warsha za kujenga stadi zinazopangwa kwa misingi ya masuala ya kujifunza kwa pamoja na nchi na kupitia uelekezi katika kiwango cha shirika.

UFUNDISHAJI
UANDAMIZI

Ujenzi wa uongozi wa wanaharakati unatolewa kupitia kuwaunganisha kwa mpango wa kujifunza wa kubadilishana wa mahirimu katika mpango wa UHAI wa wanaharakati watangulizi katika Makaazi (AiR), na kupitia ujifunzaji wenza mwingine ulimwenguni.

UWEZESHAJI
RUZUKU

Ruzuku za uwezeshaji zinafadhili malengo ya uendelezaji asasi kama vile upangaji wa kimkakati na uundaji wa sera na pia kusaidia mashirika kupanga maendeleo ya kitaalamu ya wafanyakazi wao.

Changing Faces, Changing Spaces

Changing Faces, Changing Spaces

Kupitia kufadhili na kuendesha utafiti na vile vile kongamano la Changing Faces Changing Spaces, tunaumba vifaa na nafasi za kufanikisha wanaharakati kutoa sauti kwa mazingira ya wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakzi ya ngono kwa kuwasilisha tajiriba za upangaji na utetezi, kufuatilia mielekeo na kujenga miungano na wakati huo huo kutupatia mafunzo kuhusu mabadiliko na mahitaji yaliyopo.