GRANTS

UHAI EASHRI ni ufadhili nyumbufu ambao unatoa rasilmali kwa upangaji wa wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakazi ya ngono. Tunahimiza dhana na mawazo ambayo yataendeleza mashirika haya kwa matokeo ambayo athari yake itahisiwa muda mrefu baada ya ruzuku  kuisha . Mashirika yanayoanza na yaliyokomaa yanahimizwa kutuma maombi.

GRANT TYPES

GRANT TYPES

Ruzuku za UHAI zinaamuliwa na wanaharakati wa kijamii kutoka ndani ya mashirika ya wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakazi ya ngono.

Kama mwitikio wa mahitaji ya mashirika, UHAI inatunza Ruzuku Mahirimu kupitia kwa mwito wa maombi wa mara moja kwa mwaka na Ruzuku za Fursa, Kimkakati na Uwezeshaji kwa misingi wa kuendelea .

RUZUKU MAHIRIMU

RUZUKU MAHIRIMU

Nani Anaamua

Angalau nusu ya ruzuku zote za UHAI EASHRI zinatuzwa na wanaharakati wanaoishi kwa kupigania haki za binadamu kupitia kwa mchakato wa Ruzuku Mahirimu. Tunatuza Ruzuku Mahirimu mara moja kwa mwaka kupitia kwa mchakato wazi, shindani na wa kiushirikishi unaoamuliwa na Kamati ya Ruzuku Mahirimu [PGC] ambao ni wanaharakati kumi na watatu [13] wanaoteuliwa kutoka kwa mashirika ya wafanyakazi ya ngono na wachache wa ujinsia na jinsia katika Afrika ya Mashariki ili kuwakilisha uanuwai wa kanda hii.

Tangu 2009, UHAI EASHRI imekuwa na mizunguko 13 ya Ruzuku Mahirimu na kutoa idadi fulani ya ruzuku ambazo zimetuzwa na PGC.

Ruzuku za Msingi (Hadi $5,000)

Hizi ni ruzuku za mbegu msingi za mwaka 1 na zinazonuiwa katika kuanzisha kazi mpya na /au kusaidia jitihada za kiwango kidogo. Ruzuku za Msingi zinapatikana kwa vikundi ambavyo vimefadhiliwa awali na mashirika ambayo hayajafadhiliwa awali na UHAI.

Ruzuku za Tujenge (Hadi $15,000)

Hizi ni ruzuku za mwaka 1 zinazonuiwa kuanzisha au kuchangia mipango inayoendelea, na/au kutimiza gharama za ufadhili wa kimsingi wa mashirika yanayoinuka.

Ruzuku za Imarisha (Hadi $50,000)

Hizi ni ruzuku za miaka miwili za ufadhili wa utendakazi msingi ambazo zinatolewa kwa kiwango cha juu zaidi cha 25,000 kwa mwaka. Zinanuiwa kujenga na kuendeleza mashirika yaliyo na shughuli za pana na za muda mrefu.. UHAI EASHRI ilianzisha Ruzuku za Imarisha kama mwitikio wa majibu kutoka kwa waruzukiwa wabia kwamba, wakati ambapo wafadhili wanaweza kufadhili shughuli, wafadhili wachache walikuwa wanapendelea kufadhili gharama kuu na za utendakazi wa mashirika. Ruzuku hizi ni kwa usaidizi wa kimsingi wa mashirika pekee.

Ruzuku za Fursa , Kimkakati na Uwezeshaji

Ruzuku za Fursa , Kimkakati na Uwezeshaji

Ruzuku hizi zinapatikana mwaka mzima na ni nyumbufu zaidi katika kiasi na kipindi. . Ruzuku za Fursa , Kimkakati na Uwezeshaji zinazingatiwa na Kamati ya Ruzuku ya Ukatibu[SGC] ambao unajumuisha wafanyakazi wa UHAI EASHRI na kuidhinishwa na Wakurugenzi Wakuu Wenza wa UHAI EASHRI.

Mashirika yanaweza kutuma maombi ya Ruzuku za Fursa , Kimkakati na Uwezeshaji na UHAI inaweza kuitisha maombi haya vilevile.

Ruzuku za Kimkakati

Ruzuku za Kimkakati ni ruzuku lengwa, zisizo na ushindani ambazo zinaanzisha ubia pamoja na asasi katika kuunga mkono kazi ambayo ni kubwa kimazingira na kiathari kuliko ambavyo ingekuwa katika mchakato wa Ruzuku Mahirimu . Ruzuku za Kimkakati ni nyumbufu katika kiasi na kipindi .

Ruzuku za Fursa

Ruzuku za Furasa zinatoa usaidizi wa kidharura kwa usalama, ulinzi na kesi na utetezi wa dharura na matukio mengine ya dharura ambayo hayatarajiwi katik ampango wa kikazi wa shirika. Hizi sio ruzuku za iusaidizi wa moja kwa moja wa watu binafsi kwa sababu hatufadhili watu binafsi; lakini tunafadhili mashirika ambayo yanaweza kufadhili watu binafsi.

Ruzuku za Uwezeshaji

Ruzuku za Uwezeshaji zinatoa rasilmali lakini sio tu pekee za uundaji wa stadi katika uongozi, upangaji na mahitaji ya maendeleo ya kiasasi ambayo yameundwa kimahsusi kwa shirika ili kuimarisha mifumo, miundo na michakato ili kufikia uwezo wa kiufundii kama vile maendeleo ya kiasasi, Uimarishaji wa Bodi na wafanyakazi, uwezo usio wa kiufundi kama vile kujifunza kwa mahirimu na kuunda mitandao. Ruzuku za uwezeshaji zinatolewa katika mwaka mzima na ni nyumbufu katika kipindi lakini zina kiwango cha juu cha USD 5,000.

WHAT DO YOU CONSIDER

WHAT DO YOU CONSIDER

UHAI EASHRI inawekea kipaumbele mashirika ya kiraia yanayoongozwa na kusimamia wa wafanyakazi ya ngono na wachache wa ujinsia na jinsia , lakini pia tunazingatia maombi kutoka mashirika ya kawaida ambayo yanaonyesha uhusika wa kimaana wa jamii zetu katika kufanya maamuzi na ambayo mipango yao yana athari pana na ya moja kwa moja kwa mashirika yetu.

FAQ's

UHAI EASHRI prioritises funding to civil society organisations led and managed by sex workers and sexual and gender minorities, but we also consider requests from mainstream organisations that demonstrate meaningful engagement of our communities in decision-making, and whose programmes have a direct, large-scale impact on our movements.

 • Ikiwa pendekezo langu limefanikiwa, je ni wakati gani ambao shirika linaweza kutarajia kupokea fedha?

  Ikiwa ombi lako limefanikiwa na umetutumia stakabadhi zote za kutuma maombi, utapokea ufadhili ndani ya wiki mbili baada ya kutia sahihi stakabadhi za ruzuku  ambazo idara ya usimamizi wa ruzuku itakutumia kwa nia za kimkataba. Hakikisha kwamba tuna anwani sahihi na inayofanya kazi ya barua pepe kwa mawasiliano.

 • Je utoaji ruzuku wa UHAI EASHRI ni wa kimaudhui?

  Hapana. UHAI EASHRI  ni nyumbufu na  inaitikia. Hatuamui kimbele vipaumbele vyetu vya ufadhili. Tunafadhili kwa kuitikia mahitaji ya sasa yanayobainishwa katika wakati moja hadi mwingine na mashirika yetu katika maombi mbalimbali ya ufadhili . Tunasalia wazi kwa ufadhili wa kazi za aina mbalimbali kwa kuitikia uanuwai wa maombi yanayotokana na mashirika yetu   mwitkikio is flexible and responsive.

 • Je, watu binafsi wanaweza kutuma maombi?

  Hapana . UHAI EASHRI  inafadhili tu mashirika. Hata hivyo, ikiwa kama mtu binafsi una wazo bunifu, tunamhimiza aungane au ashirikiane na shirika ambalo lipo.

 • Je, shirika ambalo halijasajiliwa linaweza kutuma maombi?

  Ndio . Tunafadhili mashirika yasiyosajiliwa kupitia wadhamini wa kifedha ambao wao wenyewe wanawachagua. Pia tupo ili kusaidia mashirika yasiyosajiliwa kumtambulisha mdhamini wa kifedha anayefaa. Mdhamini wa kifedha anapaswa awe mshirika mruzukiwa wa UHAI EASHRI,  na utoaji wao wa ripoti na wa uhasibu kwa ufadhili wetu unapaswa kuwa  wa kiwakati.