Activist In Residency

Activist In Residency

Mpango wa Mwanaharakati katika Makaazi unatoa nafasi kwa watu binafsi kutoka kwa mashirika kupata muda nje kutoka kwa kazi zao za kila siku ili kuangazia kuhusu mikakati yao kwa kutegema ujifunzaji unaopatikana kwa kuwekwa katika mashirika yaliyo sawa na yao kwa msingi wa mikatiikati na mitazamo ya upangaji kwa kipindi cha wiki kumi (10).


Mchakato wa AIR unajengwa kwa majibu kutoka kwa wabia waruzukiwa ambao wanatambulisha mahitaji yao ya kujifunza na ambapo maarifa na stadi zinaweza kupatikana ndani ya mahirimu wao. Uhawilishaji wa mafunzo yanayopatikana kwa mashirika yao baada ya makaazi yao yanajumuishwa katika ujenzi wa mpango huo. UHAI inatoa ruzuku ili kufanikisha ujifunzaji huu na vile vile utekelezaji wa mafunzo yanayopatikana.


Mpango wa Mwanaharakati kwenye Makaazi unaamini kwamba ujenzi wa uwezo fanisi ndani ya waruzukiwa unafanyika wakati kuna nafasi za uundaji wa mitandao ya mahirimu kwa mahirimu, ulezi na ubadilishanaji wa habari na utekelezaji wa mafunzo yaliyopatikana .