ABOUT
UHAI EASHRI
UHAI EASHRI ni ruzuku ya uanaharakati ya kwanza ya kiasili ya Kiafrika inayofadhili haki za binadamu za wachache wa jinsia na ujinsia. Tumefadhili kesi muhimu za korti na kugeuza sheria kandamizi, kufadhili kliniki za mwanzo za kijamii zinazohusu VVU na kufadhili jamii kuandika kuhusu maisha , upangaji na utetezi wao.
Ilianzishwa mwaka 2009, na makao yake ni Nairobi ambapo tunafadhili upangaji wa uanaharati katika nchi saba za Afrika ya Mashariki—Burundi, Jamhuri ya |Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda— na mashirika ya Kiafrika yanayofanya kazi katika bara.
Kutoka ufadhili hadi uwezeshaji hadi utafiti na mikutano tunafadhili jitihada zinazojenga maarifa, ufanisi, uwajibikaji, uendelevu na uadilifu katika jamii zetu .
Ni kitu gani kinachotufanya kuwa tofauti?
Tunaongozwa na kuamuliwa na wanaharakati ambao wanaishi maisha ya kijamii ya kung’ang’ania haki za kibinadamu kila siku. Kwa njia hii wanaharakati wa kijamii hawafaidi tu kutokana na ruzuku zetu bali pia wanaamua kuhusu ruzuku zetu.
Mnamo 2007, kongamamo la wanaharakati lenye maudhui “Changing Faces Changing Spaces” (CFCS) liliendeshwa na wachache wa ujinsia na wafanyakazi ya ngono , marafiki na wafadhii wao. Mkutano huu ulitambua tofauti zisizoweza kutatuliwa baina ya ulimwengu wa kifedha unaoathiriwa na umagharibi na ulimwengu wa kazi katika kanda hii . Hitimisho ya mkutano ulikuwa kwmba palikuwa na haja ya kuwa na utaratibu wa ufadhili unaoongozwa na wanaharakati wa kijamii ndani ya mashirika ili kuweza kuziba pengo baina ya ufadhili na kazi. UHAI ilianzishwa 2009 baada ya miaka miwili ya wanaharakati, marafiki na washauri kujengelea dhana ya utaratibu wa ufadhili unaoongozwa na wanaharakati.
Kuwa ruzuku inayoongozwa na wanaharakati ambayo ni bunifu, inayofikiwa, jumuishi na inayoitikia na ambayo inafanya kazi ili kufikia usawa, ustaarabu na haki kwa wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakazi ya ngono katika Afrika ya Mashariki na wakati huo huo kuhusika kikamilifu katika miungano ya Kiafrika.
Kuishi na kukumbatia mapenzi ya kimapinduzi
Hatusaidii tu uwanja wa haki za binadmu za wachache wa ujinsia na ujinsia na wafanyakazi ya ngono wa Afrika ya Mashariki – sisi ndio uwanja wenyewe. Wafanyakazi wetu, Bodi na kamati ya ruzuku mahirimu wanatokana na mashirika tunayofadhili na kwa hiyo ujuzi na maarifa ya mashirika yetu yanaumba na kuongoza michango yetu.
Katika utoaji wetu wa ruzuku, uwezeshaji, utafiti na mikutano, tunaumba nafasi kwa washiriki waruzukiwa kushirikiana na kujenga miungano madhubuti ya kudumu.
Ruzuku ya kwanza ya aina yake katika Afrika, UHAI imekuwa sehemu ya muungano wa wafadhili na wanaharakati wa Afrika ya magharibi ambao walitekeleza utafiti ili kufahamisha mahitaji ya kuanzisha ruzuku sawa ya kiasili ya wanaharakati wa waachache wa ujinsia na jinsia, Initiative Sankofa d’Afrique de l’Ouest (ISDAO), ambao sasa sisi ni wadhamini wake.
Mtazamo wetu wa utoaji ruzuku shirikishi ni muhimu kwetu kwa sababu:
Ushiriki ufaao katika utoaji ruzuku unaendeleza uanuwai na ujumuishi katika meza ya kufanya maamuzi kwa kuhkikisha kwamba jamii zote husika wako katika meza ya kufanya maamuzi na hivyo huwa na uwazi na huimarisha heshima kwa maamuzi ya ruzuku. Mwishowe mchakato huu hujenga ujuzi wa kitaalamu na wa uchangishaji fedha wa wanaharakati wanaohusika.
Utoaji ruzuku shirikishi ni kubadilisha uso wa msaada na kuipanua katika ngazi za kilimwengu. UHAI ni sehemu ya kikundi msingi ya watoaji ruzuku shirikishi wa kimataifa ambao walitayarisha mwongozo wa kilimwengu kuhusu utoaji ruzuku shirikishi.
Thamani zetu zinawasilishwa na maneno ya Kiswahili ambayo yanajenga jina letu. UHAI inaongozwa na ahadi kadha zisizovunjwa na ambayo yanaeleza sisi ni kina nani na ni kaida zipi zinaongoza utendaji wetu.
Michakato wazi na nyumbufu ya kujifunza, kuulizana kwa pamoja na ushiriki unajengwa kutokana na fahari na heshima ya uanuwai wetu wa ajabu. Wakati huo huo hasira na mapenzi zinasukuma kazi yeny usikivu, ushupavu na ya kimageuzi ambayo inalisha shirika lililojaa moyo na roho..
Kama watu waliotengwa, mengi ya mahitaji yetu kibinadamu na kiafya hayashughulikiwi kikawaida na kwa hiyo tunajitolea kuchukua hatua za hatari ambazo zinawezesha usaidizi nyumbufu na unaofikiwa ili kuhakikisha ustaarabu wetu wa kibinadamu . Tunapingana na chukulizi ili kujenga njia mpya za kujipanga, kufanya kazi na kuishi.
Tunaamini jamii ni wakala wake wa kibinafsi wa mabadiliko na masuluhisho yanapaswa kuongozwa na tajiriba ambazo watu wamepitia na hivyo kutuongoza katika kuchukulia ushirikiano wote kwa kujitolea kwa thamani yake na faida ya michango ya kibinafsi . Hii inajumuisha kuwafikia watu kutoka katika kitovu hadi katika maeneo ya pembeni na kujumuisha wale ambao mara nyingi wananyamazishwa na miundo ya mamlaka inayozuka.
Kwa sasa, UHAI ina Bodi wanaharakati 6 wa Afrika ya Mashariki kutoka kwa mashirika ya wachache wa ujinsia na jinsia na wafanyakazi ya ngono na Wakurugenzi Wakuu Wenza 2 ambao ni katibu wa bodi . Bodi inatawala na ina wajibu wa kifedha kwa UHAI. Hii inamaanisha kwamba wanahakikisha kuwa UHAI inatimiza wito na malengo yake. Bodi inatimiza wajibu huu wa kiusimamizi na jukumu la ufuatilizi kwa kujifahamisha kuhusu shughuli za UHAI na kufanya maamuzi ya kutuongoza kufikia mafanikio. Bodi inaidhinisha mabadiliko katika sera ya UHAI na kivyake inachagua na kualika wanachama wa Bodi wa awamu mbalimbali.
Timu yetu inajumuisha wanaharakati wataalamu wanaoajiriwa kutoka na wanaowakilisha uanuwai wa wachache wa ujinsia na jinsia katika Afrika ya Mashariki , wafanyakazi ya ngono na wafanyakazi wa mashirika wenza wa UHAI.
Cleopatra Wambugu
Director of Programmes
Wilfred Louis Mwangi
Afisa wa Mipango: Usimamizi wa Ruzuku
Jackson Otieno
Afisa wa Mipango: Utoaji wa Ruzuku
Mercy Otekra
Msaidizi wa Mipango : Usimamizi wa Ruzuku
Irene Moloney
Meneja wa Fedha ana Utendakazi
Elijah Njagi
Afisa wa Fedha : Usimamizi wa Uhasibu
Salama Nyirahabimana
Afisa wa Fedha Finance Officer: Ulipaji na Utiifu
Lynette Doreen
Msaidizi wa Utendakazi
Dennis Mwaurah
Msaidizi wa Kifedha
Chepkwemoi Kimtai
Msaidizi wa Ubia na Mawasiliano
Roselyn Odoyo
Afisa wa Mipango: Maarifa, Tathmini na Kujifunza
George Mwai
Meneja wa Mipango ; Uwezeshaji
There are no vacancies currently. Sign Up for Vacancy announcements